UHAKIKI WA TAMTHILIYA YA ORODHA

 


UHAKIKI WA TAMTHILIYA YA  ORODHA

MWANDISHI: STEVE REYNOLDS

MCHAPISHAJI: MACMILLAN AIDAN L.T.D

MWAKA : 2006

ORODHA:  Ni tamthiliya iliyotafsiriwa kutoka lugha ya kiingereza

“THE LIST”

§  Tamthiliya  ya orodha inaonyesho  moja lenye sehemu ishirini (20)

 

§  Kimsingi tamthiliya hii inazungumzia ugonjwa hatari wa UKIMWI hasa sehemu za vijijini.

 

§  Mwandishi ametumialugha ya taswira katika jina la kitabu   “ORODHA”kuonesha orodha ya mambo ya msingi ya kuzingatia ili kuepuka ugonjwa wa UKIMWI nap engine kuonesha ORODHA ya watu walioambukizwa ugonjwa wa UKIMWI

 

§  Msanii ameonesha muhusika mkuu FURAHA aliyekuwa amelelewa katika familiya yenye maadili mazuri. Furaha alikuwa na umri wa miaka 13 – 19  lakini baabaye anaonekena kuyumbishwa na rafiki yake aitwaye Mary ambaye alikuwa Malaya na ni mlevi . Kutokana na ukali wa baba yake Furaha haikuwa rahisi kwa Furaha kutoroka anashauriwa na Mary kuwa njia rahisi kutoroka kwa kupitia dirishani. Furaha alikuwa analala na mdogo wake ila kutokana na vitisho alivyopata kutoka kwa Furaha hakuweza kutoa ile siri ya Furaha kuruka kwenye dirisha ili kwenda kujivinjari na wafanyabiashara wakubwa pale kijijini kama vile bwana Ecko na Bwana Juma, siku moja wanakijiji 1 – 3 ( majirani) walipeleka taarifa mbaya kuhusu Furaha kwa wazazi wake ila mama yake Furaha alimwamini mtoto wake sana hivyo hakukubaliana nao.

 

§  Wakati huohuo Furaha alikuwa na rafiki yake wa kiume aitwaye Salim na baadaye kijana wa mtaa aitwaye Kitunda anamtongoza Furaha hivyo wanakuwa na mahusiano ya kimapenzi.

 

§  Kweli akili ni nywele kila mtu anazake kwani pamoja na Mary kumshawishi Furaha kujiingiza kwenye maswala ya NGONO Mary alitumia kinga (Kondom) ila Furaha hakutumia kinga yoyote ile na ghafla jina la Furaha linabakia kuwa huzuni kwani anapata ugonjwa wa UKIMWI.

 

§  Siku moja Furaha anakwenda kanisani ili kutubu dhambi zake hivyo anakutana na mtumishi wa Mungu aitwaye PADRI JAMES. Furaha anataja dhambi zake za ulevi na uzinzi.Padri James anamwambia Furaha kuwa dhambi zako ni nyingi hivyo uje kesho saa moja katika chumba change cha kujisomea, nyuma ya nyumba ya kanisa. Padri anamueleza Furaha kuwa mlango utaukuta uko wazi, katika hospitali ya kijijini pale daktari toka mjini anakuja kuchukua vipimo na kuwaletea wagonjwa majibu.

 

§  Majibu ya Furaha na kuonesha kuwa ameathirika na virusi vya ukimwi.

 

§  Anamweleza mama yake na baba yake na kukiri makosa yake. Furaha kabla hajafariki anaandika ORODHA inayowachanganya watu huku akimsihi mama yake aisome siku ya mazishi yake. Bwana Ecko, Bwana Juma, Salim, Kitunda na Padri James wanapata habari kuwa Furaha amefariki ila ameacha ORODHA .Wote hawa wanafanya jitihada za kuzuia orodha isisomwe kuwa na wao huenda ikawa wako kwenye orodha hiyo.

                    MAUDHUI

Tamthiliya hii ya ORODHA inazungumzia tatizo la ugonjwa wa UKIMWI vijijini Afrika.

Mwandishi amekusudia kufanya utafiti kuwa ni jinsi gani UKIMWI haupo vijijini ila mjini.

v  Mwandishi anatumia Furaha na mama Furaha alihasa kuvunja ukimya uliopo miongoni mwa jamii kutangaza hadharani kuhusu maambukizi ya ugonjwa wa UKUMWI.

v  Hili linajidhihirisha pale anapoandika orodha ya mambo ya kuzingatia ili kujiepusha na UKIMWI .Mambo hayo ni:- ni matumizi ya kondomu, uadilifu, uwajibikaji, ukweli, kuepuka unyanyapaa, upendo,msamaha, uwazi, uelewa na elimu.

v  Hivyo mwandishi anazungumzia namna watu wanavyopata maambukizi, dalili na hatua za kuchukua ili kupambana.

 

                DHAMIRA

          DHAMIRA KUU – MAPAMBANO / VITA DHIDI YA UGONGWA WA UKIMWI

          -Mwandishi katika kueleza tatizo hili la UGUNJWA WA UKIMWI anamtumia mhusika mkuu 

           FURAHA ambaye anajiingiza katika masuala ya ulevi, starehe na ushirikiano wa kimapenzi na

wafanyabiashara  Bw Ecko na Bw Juma bila kutumia kinga. Furaha anasema:-

 

                Katika ukurasa unaofuata kuna orodha ya vitu ambavyo vilisaidia kuyafupisha maisha

Yangu orodha ambayo inaonesha kwenu vyote ni kweli juu ya kifo changu ……...kondom,

uaminifu, elimu, uelewa, uwazi, uadilifu, uwajibikaji, ukweli, upendo na msamaha

…………..ukosefu wamambo yote haya ndio ulioniua (kur 44 – 45)

 

 

DHAMIRA NDOGONDOGO.

 

1.        HALI NGUMU YA UCHUMI

*Msanii anaonesha jinsi wasichana wanavyojiingiza katika vishawishi kutokana na umaskini.

Hili linajidhihirisha pale Mary anapomwambia Furaha.

 “Kuwa mwema kwa Ecko, Anaweza kukununulia vitu vingi sana. Unadhani wasichana

wadogo kijijini hapa  wanapataje viatu vipya, magauni na mabegi mapya ili

wapendeze……Wapendeze kiasi cha kuvutiavijana wazuri wa kiume? (Uk /28).

 

-Hivyo mwandishi anaona kuwa vita dhidi ya UKIMWI iende sambamba na vita dhidi ya

umaskini.

 

2.      UJINGA: Mwandishi anaona kuwa wananchi wa vijijini hawana elimu ya kutosha kuhusu ugonjwawa UKIMWI: Hili linajidhihirisha pale mwandishi anapotuonyesha mazungumzo ya wanakijiji.

               Mwanakijiji    1:   Bi Furaha anaumwa sana …….

Mwanakijiji     2:Tulijua anaumwa

Mwanakijiji   1:    …….Katubu katika ofosi ya daktari kasema ana ugonjwa wa 

AIDS  wanauita SLIM kwasababu ugonjwa unakufanya ukonde.

              Mwanakijiji        3: Lakini amewezaje kuupata ugonjwa kama huu

              Mwanakijiji        1:    Rahisi !kuna mtu kamroga………….pengine rafiki msichana 

mwenye wivu (Uk 25)

Hivyo basi mazungumzo ya wanakijiji yanaashiria kuwa watu wengi hawajui lolote kuhusiana na ugonjwa wa UKIMWI kwani wengi wanafikiri kuwa ugonjwa wa UKIMWI unatokana na kugusana na kurogwa.

3.      UWAJIBIKAJI – Wazazi wa Furaha wanawajibika kulea familia lakini Furaha anaingiwa na tama hivyo kuacha kusikiliza maonyo ya wazazi. Padri James naye hawajibiki kwa waumini wake kwani anafanya mapenzi na Furaha baada ya Furaha kwenda kutubu dhambi za uzinzi  hivyo Padri anamrubuni Furaha na kuzini naye usiku. Mwandishi anatuonyesha mazungumzo  ya Furaha na Padri James.

 

4.      MMNYOKO  WA MAADILI

-Mwandishi anamchora Furaha jinsi alivyokuwa amelelewa katika maadili mazuri ila baadaye anajiingiza katika maadili mabaya kama vile:- kunywa pombe/ulevi, uvutaji bangi, uasherati na umalaya. Baba yake Furaha anasema.

 

“Nilichokuwa nafahamu …………hadi sasa Furaha ...........ni kwamba amekuwa

akitoroka nyumbani wakati wa manane!.......kutoroka…ruhusa….baa……….wanaume

wewe…..malaya usiye na shukrani ! “ (Uk 11)

-Viongozi wa dini kama Padri James hakuwa na maadili mema pale anapomchanganya Furaha kuzini naye.

 

5.      UNAFIKI

Msanii ameonyesha kuwa viongozi wa dini wanafiki kwani wanavyosema sivyo wanavyotenda.

Furaha ni mnafiki kwa wazazi wake (Uk 5,8) anaomba msamaha lakini haachi vitendo viovu.

-Bw. Ecko ni mnafiki kwa mkewe kwani haheshimu ndoa yake.

 

    6.    HUDUMA DUNI ZA AFYA. Msanii anaonesha kuwa huduma za jamii ziko mbali sana na

makazi ya watu hivyo Furaha alishindwa kwenda ili kupata matibabu. Mama yake furaha

anasema.

   “……Daktari kutoka wa karibu alifika na kuchukua sampuli ya damu ili kupima

malaria……….(uk 23)

          Hivyo basi anaashiria kwamba vijijini hakuna huduma bora za afya hivyo ni vigumu kupambana 

na ugonjwa wa UKIMWI.

 

7.      UWAZI NA UKWELI- Msanii anaona kuwa ili kupambana na kushinda ugonjwa wa UKIMWI ni lazima jamii kuwa wakweli Padri James, Bw Ecko, Bw Juma, Salimu na Kitunda hawakuwa wakweli. Ila mwishoni  Furaha anavunja ukimya na kusema kuwa ana UKIMWI.

 

8.      UPENDO – Msanii anataka jamii nzima kuwa na upendo kwa waathirika wa UKIMWI. Mfano Mama Furaha na Furaha walikuwa na upendo.

 

9.      ULEVI – Msanii anaona kuwa ulevi ni tatizo kubwa kwani huwafanya watu wasiweze kujitawala hivyo kupata ugonjwa wa UKIMWI.

10.  MALEZI – Hapa msanii anashauri kuwa malezi ya jamii nzima wala siyo wazazi peke yake kwani majirani wa akina Furaha (Wanakijiji 1 – 4) walikuwa wanaleta  taarifa mbaya za Furaha ila wazazi wake hawakuamini kabisa .

 

11.  MAPENZI NA NDOA  - Mwandishi anaona kuwa yapo mapenzi ya  ukweli nay a uongo mfano Salimu na Furaha, mama yake Furaha na Furaha walipendana sana.

-          Mapenzi ya ulaghai ni ya Padri James, Bw Ecko na Juma Kitunda

Mwandishi anaona kuwa hakuna uaminifu katika ndoa.

XXXXXMCHAMBUZI MWL MKAMBA. BAED (HONS) UDMS 2009XXXXX

 Inaendelea=======>

Share on Google Plus

ABOUT BLOGGER MKAMBA EDUCATION CONSULTANCY

Hi! I am Zachary John Bequeker, from Mwanza Tanzania, East Africa.I'm a blogger of ZAKACHEKA NEWS LINE And ZAKKACHEKA INJILI.Contact me +255 625966236 / +255 758590489 or mail on zacharybequeker@gmail.com . Thanks!!!

0 Post a Comment:

Post a Comment