UHAKIKI WA RIWAYA
TAKADINI
2004
MWANDISHI
– BEN J. HAMSONI
MCHAPISHAJI
– MATHEWS BOOK STORE AND STATIONERS
Riwaya hii ya TAKADINI
inahusu mila na desturi za kiafrika hasa za kuua MAALBINO (watu wenye ulemavu
wa ngozi).
*Mwandishi ameonesha
jinsi mila hizi zilivyopitwa na wakati na kutaka jamii za kiafrika ziachane na
mila hizi kwani hurudisha nyuma maendeleo:
Mwandishi anaonesha
jinsi Sekai alivyo a mzaa TAKADINI (SOPE) na kusababisha atoroke katika kijiji
kile ili kumnusuru Takadini asiuwawe.
1.MAUDHUI
DHAMIRA KUU – UKOMBOZI
WA KIUTAMADUNI
Mwandishi anaonesha
jinsi jamii zinavyokumbatia mira na desturizilivyopitwa na wakati hasa zile
zinazomkandamiza mwanamke na mtoto katika ndoa, mirathi, utu, elimu uhai
maamuzi, magawanyo ya kazi na mapato.
Mwandishi anaeleza
jinsi jinsi mila hizi potofu zinavyohatarisha maisha ya watoto walemavu kama
Takadini, kijana aliyezaliwa akiwa zeruzeru ambaye jamii yake iliazimia kumuua
siku ya pili baada ya kuzaliwa mwandishi anasema.
“Sekai alimpenda Makwati siku zote,
na sasa anamuacha aamuliwe na wazee kwa sababu
ameshindwa
kumpatia aina ya mtoto yetaka ……. Katika kijiji hiki zeruzeru hakuwa na nafasi
(uk 12) “
Hapa
tunaona jinsi wazee wa kijiji hiki walivyokuwa wasimamizi wakuu wa mila na desturi mbaya hali iliyosababisha
Sekai atoroke ili kuponya maisha ya Takadini yasiangamizwe nay eye pia kama
Makwati anaposema.
“Lakini Sekai endapo wataamua
mtoto auwawe hata nay eye atauawa kwa sababu ya
kupinga
sheria za kale “
Hivyo
basi hatuna budi kuachana na mila zilizopitwa na wakati na kuanza kutetea haki,
uhuru na utu wa watu dhidi ya mila na desturi.
Mwandishi
anamuonyesha Sekai jinsi anavyokuwa jasiri kwa kupinga mila potofu zilizopitwa
na wakati kwa kutoroka na Takadini ili kukwepa adhabu ya kifo ambayo wangeipata.
“Sekai alikwisha amua
lazima aondoke asubuhi itakayofuata kulilia uhai wa watoto wake”
Pia
msanii anaonesha jinsi mila na desturi zinavyojitokeza kwenye ndoa pale Shingai
anapochaguliwa mtu kumuoa.Wazazi walimkatalia asiolewe na Takadini ila aolewe
na Nhano mvulana jasiri lakini msichana huyuhuyu anataka kuchaguliwa mtu wa
kumuoa na wazazi wake na kuolewa na Takadini.
Msanii
anamchora Shengai akiwaeleza wazazi wake :-
“Huyu ndiye mtu anayetaka
anioe, wewe na baba mlikuwa na hamu ya kuniozesha kwa nyumba ya Manyamombe
hafuati matakwa yangu hayakusikilizwa (uk 118)
Hivyo
mwandishi anaonyeshaa kuwa ni sisi wenyewe tunaotaka kupambana na mira na
desturi zilizopitwa na wakati kama Shingai na Takadini walivyoleta mabadiliko
katika jamii . Tendai anashuhudia hilo na kusema.
“Wewe
na Takadini mmebadilisha mambo mengi kijijini hapa kwa sasa sifikirii kwamba
kuna mtu yoyote atakayekuwa na moyo wa kuwaharibu watoto wachanga masopeau
wenye ulemavu. Ahsante nyinyi kwako na Takadini kwa baba Chivero (uk 126)
Hivyo
msanii anaonesha jinsi watu wanavyotakiwa kupinga mila potofu ili kuleta
ukombozi katika jamii.
DHAMIRA
NDOGONDOGO
1. NDOA.
Ni makubaliano kati ya watu wawili wanaokubaliana ila tunaona mila na desturi
zinaingilia
maswlawa
ya ndoa.
Shingai analazimishwa kuolewa na
Nhamo wakati Shingai alikuwa hampendi pale anaposema
“Nataka waniache peke yangu ili
niamue mwenyewe (uk115)
2. MAPENZI.Katika
riwaya hii kuna mapezi ya kweli nay a uongo.
Mapenzi ya dhati kati ya
Takadini na mamae, Takadini na mzee Chivero, Takadini na
Shengai, Sekai na Pindai na
Sekai na Mzee Chivero. Shengai anasema kuwa” huyu ndiye
mtu
ninayetaka anioe…. Wewe na baba mlitaka kuniozesha katika familia ya Manyambe”
(uk118)
Sekai alimpenda Takadini
hasa pale anapomwambia makwati kwa………………
“Ni mtoto wangu wa
kwanza niliyemsubiri kwa miaka mingi siwezi kukubali
kumpoteza
la humtaki nirejeshe kwetu nitajitoa mhanga kwa ajili yake” (uk 11)
Chiveri
alimkaribisha Sekai katika kijiji chake . Chivero na Takadini walipendana sana
kwani alimfundisha namna ya kufahamu mitishamba na uwindaji.
Ø Mapenzi
ya uongo ni kati yam zee Makwati kwa Sekai baada ya kujifungua mtoto zeruzeru.
Ø Mapenzi
kati ya Dadirai na Bumbidzui kwa Sekai jinsi walivyokuwa wakimsengenya.
3.DHANA
POTOFU
Jamii
nyingi za kiafrika zinaamini mila potofu zilizopitwa na wakati ikiwa ni pamoja
na kuwaua zeruzeru mfano Mapunzure anasema “matoto lazima auwawe” (uk 35)
4. UMOJA NA USHIRIKIANO
Mwandishi
anasisitiza kuwa ili kupiga vita mila potofu ni lazima kuwa na umoja na
ushirikiano. Mzee Chivero, Tendai na Mtemi Masasi walishirikiana kumlina
Takadini dhidi ya unyanyapaa. Mzee Makwatianasema “sasa kinajua sope hawezi
kuzaa sope”
5.UJASIRI
Msanii
anasema ujasiri ni silaha mojawapo katika kuleta uokombozi dhidi ya mila potofu. Mfano Sekai alikuwa jasiri
kutoroka ili Takadini asiuawe, Shengai alikuwa jasiri kukataa kuolewa na Nhamo
(Mchumba aliyechaguliwa na mzazi wake)
0 Post a Comment:
Post a Comment