UHAKIKI WA TAMTHILIYA
TAMTHILIYA: NGOSWE PENZI KITOVU CHA
UZEMBE
MWANDISHI: EDWIN
SEMZABA
MWAKA: 1988
MCHAPAJI: DAR ES SALAAM
UNIVERSITY PRESS
UTANGULIZI
Ngoswe penzi kitovu cha uzembe ni tamthiliya
inayochambua haki halisi ya kijijini namna watendaji wanavyoshindwa kuwajibika
katika kuleta maendeleo ya kijamii sehemu za vijijini .
Mwandishi
anaonesha namna Ngoswe anavyoharibu kazi ya sense kwa uzembe wake wa
kuchanganya mapenzi na kazi pia anaonesha hali duni za maisha katika sehemu za
vijijini, kukosekana kwa huduma kama vile shule, hospitali ni kikwazo kikubwa
sana katika maendeleo.
MAUDHUI
DHAMIRA KUU:KUCHANGANYA
MAPENZI NA KAZI
Mwandishi
wa tamthiliya hii ameliweka suala hili kuwa kitovu cha uzembe. Mwandishi
ametuonesha Ngoswe akiwa na uchu wa mapenzi mara amwonapo mazoea. Tatizo la Ngoswe
halikuwa kupenda bali kushindwa kudhibiti penzi lenyewe na kusababisha
kuharibika kwa kazi ya sense kwa kuikosesha serikali kumbukumbu za baada. Hivyo
msanii anaiasa jamii kutochanganya mapenzi na kazi kwani huwezi kuwatumikia
mabwana wawili.
DHAMIRA NDOGO NDOGO
i)
ATHARI
ZA ULEVI:
Mwandishi ametuonesha kuwa suala la ulevi ni chanzo cha uzembe kazini. Mtunzi
wa tamthiliya hii amewatumia Ngoswe na mito mingi wanaojihusisha na ulevi wa
pombe za mnazi wakati wa kufanya kazi ya sense. Ulevi huo ulisababisha uzembe
na hatimaye mito mingi anaamua kuchoma kazi ya sense.hivyo msanii anataka jamii
kuacha ulevi kwani huathiri uwajibikaji kazi.
ii)
UMUHIMU
WA ELIMU : mwandishi wa tamthiliya hii
ametuonesha kuwa watoto wengi hawasomi kwa sababu shule ziko mbali. Hivyo jamii
haina budi kujenga shule karibu ili kila mtoto apate elimu.
Vilevile mtunzi ametuonesha mitomingi
akiwa na dhana potofu juu ya elimu kwani anasema wazee wengi hawasomagi wasome
nyie vijana. Elimu haina mzee wala kijana kwani elimu haina mwisho, hivyo kila
mtu anafrsa ya kusoma.
Pia msanii anatuonesha kuwa endapo elimu itatumika vibaya, basi inaweza
kuleta madhara makubwa kwa jamii. Mwandishi ametuonesha Ngoswe aliyekuwa na
Elimu ya kutosha anashindwa kuleta ufanisi wa kazi ya sense. Hivyo ili elimu
iweze kuwa ya manufaa ni lazima itumike katika kuibadilisha na kuisukuma mbele
jamii katika suala zima la maendeleo.
iii)
IMANI
ZA KISHIRIKINA: mwandishi ametuonesha Mama jane
akikataa kuhesabiwa kwa sababu ya imani za kishirikina kwani anadai kuwa
ukituhesabu watoto wa watu ili awaroge. Hivyo msanii anaitahadhalisha jamii
kuwa imani za kishirikina hazina nafasi katika kuiletea jamii maendeleo
iv)
MALEZI
NA NDOA ZA MITARA: mwandishi wa tamthiliya hii
ametuonesha mama mazoea anajihusisha na malezi ya mazoea ingawa kulikuwepo na
mwingiliano kutokana na mitomingi kuendekeza ndoa za mitara. Hivyo kusababisha
wake zake kutokuelewana katika suala la ,alezi ya mazoea.; hivyo mtunzi anaiasa jamii kuepuka
ndoa za mitara kwani huweza kusababisha kutokuwepo kwa utulivu katika familia.
v)
ATHARI
ZA UVIVU : mwandishi wa tamthiliya hii
ametuonesha kuwa kijiji cha Ngengemkeni kinaelekea kuwa na watu wengi walevi
suala hili linaathiri kazi zote zinazohusu watu na kusababisha jamii kutokupata
maendeleo. Watu wanajihusisha na ulevi kuliko kufanya kazi, hali inayopelekea
kuwepo kwa umasikini katika jamii. Hivyo jamii lazima iachane na uvivu kwani ni
sumu ya maendeleo.
vi)
NAFASI
YA MWANAMKE KATIKA JAMII : mwandishi wa
tamthiliya hii amemchora mwanamke katika nafasi zifuatazo.
Ø Mzazi
na mlezi, mwandishi ametuonesha mama mazoea akijihusisha na malezi ya mwanae
ingawa mazoea alitoroshwa na Ngoswe. Hivyo ni jukumu la wazazi wote kuwapa
watoto wao malezi.
Ø Kiumbe
duni, mwandishi ametuonesha mitomingi akiwafananisha wakeze na mazoea kwa
kusema kuwa akili zenu ni sawa na za mazoea. Hii inaonesha kudharauliwa kwa
mwanamke tabia ambayo Haifa katika jamii
Ø Chombo
cha starehe, mwandishi amemchora mwanamke kama chombo cha starehe baada ya
kuwaonesha mitara,mfano mitomingi aliyekuwa na wake wawili. Mama mazoea na mama
mainda. Hivyo wanaume hawapaswi kuwatumia kwa ajili ya kukizi haja zao bali
wawathamini.
Ø Mwepesi
wa kushawishika; mwandishi ametuonesha mazoea anakubali kutoroshwa na Ngoswe
ilihali alikuwa na mchumba tayari. Hivyo mwandishi anaiasa jamii hususani
wanawake kuwa waaminifu.
vii) MIVUTANO YA MAADILI YA
MJINI NA KIJIJINI: mwandishi wa tamthiliya hii
ametuonesha tofauti za kiutamaduni kati ya maisha ya mjini na kijijini. Mtunzi
ametuonesha mivutano ya kimaadili, kitendo cha Ngoswe kumtorosha mazoea bila
ridhaa ya wazazi ni kinyume na taratibu za vijijini lakini ni jambo la kawaida
kwa upande wa mjini. Hivyo msanii anasisitiza maisha ya kijamaa yadumishwe
mjini ili maadili mema yatawale .
Huu ni mwelekeo wa imani ya mwandishi kuhusu
maisha. Msanii anaamini kuwa jamii inaweza kuingia katika matatizo pindi
inapochanganya vitu viwili kwa wakati mmoja. Vilevile msanii anaamini kuwa
ubora wa maisha ya watu kutokana na watu kuishi kijamaa. Hivyo ujamaa ndio
utakaomaliza matatizo mbali mbali katika jamii.
MSIMAMO /
MITAZAMO
Hii ni hali ya mwandishi kuamua kufata na
kushikilia jambo Fulani. Mwandishi wa tamthiliya hii ana msimamo wa kimapinduzi
kwani wamezungumzia wazi juu ya matatizo mbalimbali yanayoikabili jamii na
kuonesha uhalisia wake.matatizo haya ni umaskini, ulevi, elimu, ndoa za mitara.
Hivyo mwandishi anaonesha suluhisho la matatizo hayo ni kuishi kijamaa.
UJUMBE
Ni funzo ambalo msomaji wa kazi ya fasihi
hupata baada ya kusoma kazi mbalimbali za fasihi
-
Baadhi ya ujumbe katika tamthiliya ya
Ngoswe penzi kitovu cha uzembe ni
i)
Jukumu la malezi katika familia si la
mtu mmoja bali ni wajibu wa baba na mama. Hivyo wazazi wote wawili wana jukumu
la kumlea mtoto ipasavyo. Ujumbe huu unaibua dhamira ya malezi
katika familia
ii) Ulevi
ni kikwazo cha maendeleo katika jamii. Hivyo haipaswi kuchanganya ulevi na
kazi. Mwandishi anaibua dhamira ya Athari
za ulevi
iii) Ni
vema shule zijengwe karibu ili watoto waweze kupata elimu kwa urahisi dhamira
inayotokana na ujumbe huu ni suala la Elimu
katika jamii
iv) Jamii
inapaswa kuachana na dhana ya kumchukulia mwanamke kama chombo cha starehe na
mtuduni. Ujumbe huu unaibua dhamira ya Nafasi ya mwanamke katikajamii
v) Suala
la imani za uchawi na ushirikina linatakiwa kutupiliwa mbali kwani hukwamisha
maendeleo katika jamii ujumbe huu unatupatia dhamira ya Imani zakishirikina
vi) Kupenda
si dhambi bali tunapaswa kuzingatia wakati wa kupenda, mahala na nani
anayependwa? Msanii anatuasa kuwa mshika mawili moja humponyoka kama
ilivyotokea kwa Ngoswe. Ujumbe huu unatupatia dhamira ya Mapenzi
vii) Mapenzi
yasiofuata utaratibu unaokubalika katika jamii ni chanzo cha kuharibu utendaji
wa kazi. Hii imejidhihirisha kupitia Ngoswe na mazoea hivyo kuibua dhamira ya mapenzi na kazi.
viii)
Suala la uzembe linaweza kusababisha
umaskini na kutokuendelea katika jamii. Ujumbe huu unaibua dhamira ya Athari za uzembe
ix) Ni
bora huduma za kijamii zitolewe sehemu zote mjini na vijijini, huduma hizi ni
kama vile shule, hospitali, maji na umeme. Ujumbe huu unaibua dhamira ya umuhimu wa huduma za kijamii.
MIGOGORO:
Migogoro ni misiguano/ mivutano au hali
ya kuelewana baina ya pande mbili au zaidi katika kazi ya fasihi
Miongoni mwa migogoro iliyojadiliwa katika tamthilia hii ni pamoja na
·
Migogoro kati ya Ngoswe na wazazi wa
mazoea, chanzo cha mgogoro huu kilikuwa kutoroshwa kwa mazoea na Ngoswe bila
ridhaa ya wazazi wake hivyo suluhisho la mgogoro huu ulikuwa mbaya kwani
mitomingi aliamua kuchoma kazi ya sense.
·
Migogoro kati ya mazoea na wazazi wake,
mgogoro huu ulitokea baada ya mazoea kuamua kutoroshwa na Ngoswe wakati tayari
alikuwa na mchumba hii ilikuwa kuchomwa kwa kazi ya sense na kusababisha
mitomingi kudharau wakeze kwa kusema kuwa wamechangia katika kutoroshwa kwa mazoea.
·
Mgogoro kati ya Ngoswe na serikali,
mgogoro huu ulitokea baada ya Ngoswe kuharibu kazi aliyotumwa na serikali kwa
uzembe na mapenzi suluhisho la mgogoro huu lilikuwa kufikishwa kwa Ngoswe
katika mikono ya sharia lakini Ngoswe
anaahidi serikali kuwa sense ijayo kutokuvurunda tena.
·
Mgogoro kati ya mitomingi na serikali,
chanzo cha mgogoro huu kilitokea baada ya uamuzi wa mitomingi wa kuchoma moto
kazi ya sense. Kwa sababu Ngoswe alimtorosha bintiye suluhisho la mgogoro huu
lilikuwa mitomingi kuahidi serikali kuwa hatarudia makosa hayo.
·
Mgogora kati ya mitomingi na wakeze,
mgogoro huu uliyotokea baada ya mazoea kutoroshwa na Ngoswe, mitomingi anahisi
wakeze walijua jambo hili suluhisho la mgogoro huu ulikuwa mitomingi
kuwadharirisha wakeze kuwa akili zao ni saw ana za watoto hali hii iliwa
dharirisha wakeze.
·
Mgogoro kati ya mama mazoea na mama
linda, mgogoro huu ulitokana na kuingiliana katika malezi ya mazoea kitendo
kilichosababisha mazoea kutoroshwa. Hivyo kulijengeka chuki kati ya mama mazoea
na mama mainda
0 Post a Comment:
Post a Comment