UHAKIKI WA MASHAIRI YA CHEKA CHEKA
MWANDISHI: THEOBALD A MVUNGI
WACHAPISHAJI: EDUCATIONAL
PUBLISHERS AND DISTRIBUTORS LTD
MWAKA 1995
MCHAMBUZI:
MKAMBA
Msanii wa mashairi ya chekacheka
amejadili kwa kina matatizo yanayoikumba jamii yake hasa yale ya kisiasa.
Kama vile rushwa, uhujumu, uchumi, uongozi mbaya, democrasia ya chama kimoja na
vyama vingi. Pia amejadili masuala ya mapenzi, dini, ukasuku wa waandishi na
mengineyo.
MAUDHUI
DHAMIRA KUU –
UMUHIMU WA KUWEPO KWA UONGOZI BORA KATIKA JAMII
Mwandishi ameonyesha sifa za uongozi
bora kuwa ni wale wanaosema ukweli bila uongo na bila kuwapa wahujumu uchumi
mafuta kwa mgongo wa chupa katika shairi la “kazi yetu harakati” amebainisha
kuwa viongozi bora lazima wawe wakweli.
Pia democrasia ya kweli ni ile inayojali haki za wananchi na kuwapa watu uhuru
wa kuamua mambo yao wenyewe katika shairi la taifa “wamelizika”anaetaka jamii
iwe na demokrasia ya vyama vingi badala ya chama kimoja cha siasa.
“Waogopa vingi vyama, ni hofu ya kuumbika
Maovu wanayafuma, kwa
dharau na dhikika
Vyama vingi vinasema , na
kutwaa madaraka
Pasipo
uhuru huo, utu upo mashakani.
Hivyo
msanii anatuonesha jinsi mfumo wa chama kimoja unavyficha maovu ya viongozi
katika jamii yetu. Hivyo basi msanii anataka uongozi bora wenye kukemea maovu kama vile usaliti, matabaka na
unyonyaji ili kuleta maendeleo ya kweli katika
DHAMIRA
NDOGONDOGO
1.
USALITI
Msanii
anaona kuwa kuna baadhi ya viongozi ambao ni wasaliti hasa pale wanapofunga
mali ya umma wakiwaacha wananchi wakiteseka na hali duni ya maisha katika
shairi la “kuna nini huko ndani”
msanii anasema.
‘Tumewaletea kuni, maharage hata unga,
Halafu
mnatuhiki, marafikizo mwahonga,
Mwataka
tulale chini,mturese mkiringa,
Hizo
kofia nyeupe, tumewaazima sisi.
Hapa
mshairi anawauliza wapishi kuwa wanapika halafu wanakula wenyewe.
2.
SUALA
LA MATABAKA
Msanii
ameona kuwa katika jamii yake kuna matabaka yaani tabaka tawala (viongozi) na
tabaka tawaliwa (wananchi) msanii anadhihirisha hili katika mashairi ya “utu
umekuwa kima” mashairi ya ngulu. Tabaka tawala linanyanyasa na kunyonya tabaka
la chini.
3.
UONGOZI
MBAYA
Uongozi
mbaya ni kiwazo cha kuleta mageuzi na maendeleo katika jamii.
Msanii
anaona kuwa uongoziulioko madarakani haujali wananchi na wanajilimbikiza
mali.Mashairi yafuatayo yanashadadia dhamira hii. “Chura amegundulika” “utaliwa
kama punda”, “Chunguzeni walio mbele”, muwapinawauliza?”
4.
UKWELI
NA UWAZI KATIKA JAMII
Mwandishi
anataka viongozi wakweli wasio na woga katika kuwafichua wahujumu uchumi katika
shairi la “mwinyi ume………………………katika shairi la “kweli ilojaa udi”
“Ati ni
maendeleo, mana watu wamezidi,
Hakuna kasema
siyo, kweli uliyojaa udi,
Kweli yenye
kivutio, kweli yenye ustadi,
Hukuna
dongo namito, wala watu na mipango.
Hivyo
msanii anataka viongozi kuwa wakweli hasa pale matatizo yanapotokea
wasidanganye wanamili na wametayali
kufichua maovu katika jamii.
5.
DEMOKRASIA
Msanii
anaamini kuwa demokrasia ya mfumo wa chama kimoja ni chanzo cha viongozi
kuficha maovu katika shairi la “Taifa wamelizika “ msanii anasema .
“Mmezikwa
demokrasi, chama kimoja ndoo ngao,
Watu hawana
nafasi , kutetea nchi nyao,
Mawazo ya
ukakasi, mawazo ya mtitio
Wapenda jibu
mkato, wale woga wa hoja.
“Waogopa vingi
vyama, ni hofu ya kuumbuka,
Maovu wanayotuma, kwa dharau
na dhikika,
Vyama vingi
vinasema, na kutwaa madaraka,
Pasipo
uhuru huo, utu upo mashakani.
Hapa
msanii anaonyesha jinsi viongozi wanavyoogopa mfumo wa vyama vingi. Kwa hofu ya
kuumbuka. Hivyo naamini kwamba siasa ya mfumo wa vyama vingi ndio suruhisho
pekee la matatizo nchini Tanzania.
XXXXXMCHAMBUZI MWL MKAMBA. BAED (HONS) UDMS 2009XXXXX
0 Post a Comment:
Post a Comment